Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu
Kufuatia kifo cha mwanazuoni mwanajihadi Ayatullah al Haj Sayyid Muhammad
Hussein Fadhlullah (Mwenyezi Mungu amrehemu) ninatuma rambirambi na mkono wa
pole kwa familia ya Fadhlullah, marafiki na wapenzi wa marehemu nchini Lebanon,
jamii za Walebanon katika mabara ya Afrika na America ya Latini na kwa mashia wote
wa Lebanon. Mwanazuoni huyu mkubwa aliyekuwa na bidii alikuwa na taathira
katika medani za dini na siasa, na Lebanon haitasahau huduma na baraka zake kwa
miaka mingi.
Katika kipindi chote cha umri wake harakati ya mapambano ya Kiislamu ya
Lebanon ambayo ina haki kubwa juu ya umma wa Kiislamu, imefaidika na himaya,
ushirikiano na msaada wa mwanazuoni huyo mpiganaji jihadi.
Ayatullah Fadhlullah pia alikuwa mtetezi mwenye ikhlasi na shupavu wa
Jamhuri ya Kiislamu na daima alithibitisha kwa maneno na vitendo uaminifu wake
kwa Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chote
cha miaka thalathini iliyopita.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ateremshe rehma na maghufira yake kwa
roho ya sayidi huyo sharifu na azizi na amfufue pamoja na mababu zake watoharifu.
Sayyid Ali Khamenei
Tarehe 14 Tir 1389 (05/07/2010)